Maafisa Ugani Ngazi ya Kata Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kutekeleza majukumu yao ipasasyo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Jamii.
Akizungumza na Maafisa Ugani Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndugu Robert Mwanawima Januari 17,2024 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kukumbushana ili kutekeleza yale ambayo yanapaswa kutekelezwa na kuyasimamia katika maeneo husika.
" Tupo kwenye msimu wa Kilimo mkaendelee kutoa Elimu kwa wakulima lakini pia mkatoe chanjo kwa Mifugo ili kuepuka mlipuko wa magonjwa kwa mifugo yetu ," amesema Ndg.Mwanawima
Naye Afisa Rasilimali Watu Ndugu.Raphael Mputa ametoa rai kwa Maafisa Ugani kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma katika maeneo yao huku akiwasistiza kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza majukumu yake aliyopangiwa kwenye mfumo wa PIPMIS .
Kwa upande wao Maafisa Ugani wamesema wataendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi kwenye maeneo yao ikiwa pamoja na kutoa Elimu ili kuweza kuleta tija katika Sehemu ya kilimo na mazao sambamba na Mifugo.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa