Maafisa Ugani kilimo 51 walioajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) wamepewa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kwenda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika Kata walizopangiwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba .
Akisoma taarifa ya ufunguzi wa mafunzo hayo leo Januari 13,2025 Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg.Francis Mkuti amewataka maafisa ugani hao ambao watakwenda kwenye Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuzingatia mafunzo hayo ili kwenda kuongeza uzalishaji wa zao la korosho .
" Napenda kuwapongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa usimamizi mzuri wa korosho kwa ongezeko la uzalishaji ambapo msimu huu wa mwaka 2024/2025 tumeshuhudia ongezeko kutoka Tani 310,787 mwaka 2023/2024 hadi kufikia Tani 410,000 mwaka 2024/2025 hivyo maafisa ugani hawa watakuwa chachu ya kuongeza uzalishaji lakini pia mkatumie nafasi mliyopata kuonesha uzalendo wenu kwa wakulima wetu kwa kufanya kazi kwa juhudi kubwa pia mtaongeza ujuI na kupata uzoefu wa ufikishaji wa huduma za ugani kwa wakulima ili wazalishe kwa tija mazaonwanayolima likiwemo Korosho,"
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa bodi ya korosho Ndg.Johnson Kaaya amesema mafunzo rejea ya maafisa ugani hao ni mpango wa kukuza ujuzi kwenye Programu ya Jenga kesho iliyo bora ambapo baada ya kuwajengea uwezo waende wakatekeleze kwa vitendo ili kuongeza uzalishaji wa zao la korosho.
Aidha amesema mpango wa kuajiri maafisa ugani hao ni kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi nchini kufikia Tani 700,000 mwaka 2025/2026 na Tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2029/2030. " Maafisa ugani hawa katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko chanya watakabidhiwa vitendea kazi ambavyo ni pikipiki na vishikwambi ili wakatekeleze shughuli za uendeshaji wa zao la Korosho," amesema Kaaya
Mafunzo hayo ya siku tano kwa Maafisa Ugani yatahitimishwa Januari 17,2025
#Tandahimba tumejipanga kazi zinaendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa