Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Maafisa Maendeleo ngazi ya Kata wamejengewa uwezo wa jinsi ya kutumia mfumo mpya(TPL MIS) wa utoaji wa mikopo ya asilimia kumi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambao utarahisisha upatikanaji wa mikopo hiyo
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiwa katika kikao kazi
Akifungua kikao kazi hicho leo Juni 17,2022 Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Aloyce Massau kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa mfumo huo utawawezesha wanavikundi kupata huduma katika maeneo yao waliyopo ambao utaanza rasmi Julai Mosi,2022
Ndugu .Aloyce Massau Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba akifungua kikao kazi
“Tunahama katika usajili kwa kutumia makaratasi na sasa tutatumia mfumo ambao utarahisisha mikopo kwa haraka ,maafisa maendeleo watafanya usajili katika maeneo yao ya utendaji,”amesema Ndugu Massau
Aidha amesema kuwa lengo la mfumo huu ni kuhakikisha kuwa hakutakuwa tena na vikundi hewa,hakuna mtua ataomba mkopo zaidi ya mara moja,utarahisisha utunzaji wa kumbukumbu hivyo watapata mikopo kwa haraka na watasajili vikundikwa uhakika
Naye Afisa Maendeleo kata ya Namikupa Bi.Kissa Mwakabana ameshukuru kwa kikao kazi na kueleza kuwa Mfumo huo utawawezesha kusajili vikundi katika maeneo yao na utapunguza wana vikundi kuja makao makuu ya Wilaya badala yake watapata huduma hizo katika maeneo husika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa