Na Kitengo cha Mawasiliano
Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kusimamia na kuhakikisha wanafunzi wa darasa la pili wanamudu Kusoma,Kuandika na Kuhesabu (KKK) sambamba na kusimamia upatikanaji wa lishe katika shule zao
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Robert Mwanawima wakati akizunguma na Maafisa Elimu Kata 32 na Walimu Wakuu 127 katika kikao cha Tathimini ya Ufanyikaji wa Mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi na Upimaji wa Darasa la nne mwaka 2022 kilichofanyika Novemba 12,2022 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Tandahimba
“Nawapongeza kwa kumaliza Mitihani salama,mkayasimamie na kuyatekeleza yale ambayo tumeazimia katika kikao chetu ili tuendelee kuboresha Elimu katika Halmashauri yetu kikubwa ni kuondoa tatizo la watoto wasiomudu KKK ili waweze na kuendelea darasa linguine,”amesema Ndg.Mwanawima
Aidha amesistiza Walimu Wakuu kuenddelea kutoa Elimu ya Uelewa kwa wazazi na walezi waweze kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi wote waweze kupata lishe hatua ambayo itasaidia kupunguza utoro mashuleni lakini pia itaongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa kuhudhuria vipindi kwa ufanisi
Nao Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wameahidi kuyasimamia na kuyatekeleza maazimio ambayo tumekubaliana ili kuleta mafanikio katika Elimu ndani ya Wilaya
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa