Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndugu.Rashidi Hamidu Shabani amewasistiza wananchi kutumia Wiki ya Sheria kupata Elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria na msaada wa kisheria kutoka kwa maafisa wa Mahakama ambao watatoa huduma hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tandahimba.
Hayo ameyasema leo Januari 27,2024 wakati akizindua Wiki ya Sheria akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, kwenye viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya,Watumishi,Wananchi na baadhi ya wanafunzi .
" Wananchi mjitokeze kwa wingi katika maeneo ambayo watatoa msaada wa kisheria ili mpate elimu ya.masuala.mbalimbali ya Sheria kutoka kwa Maafisa wa Mahakama,Mahakama zetu zimeboresha huduma ambapo sasa zinatumia mifumo katika utoaji wa huduma mbalimbali," amesaema Katibu Tawala.
Kwa upande wake Mhe.Joseph Waruku Hakimu Mkazi.Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba amesema wananchi katika Wiki ya Sheria watapata fursa ya kupata Elimu ikiwa pamoja na kupata msaada wa kisheria ,Uandishi wa Wosia,Usimamizi wa.Mirathi.na huduma mbalimbali.
Aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yameanza Januari 24,2024 yatahitimishwa Februari 1,2024 ambapo wananchi watapata fursa ya kuzungumza na kujadiliana na Maafisa wa Mahakama na wadau mbalimbali kwa lengo la kujifunza katika maeneo waliyotenga kutolea huduma ikiwa pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba.
Kila Mwaka hapa Nchini Tanzania huadhimisha Wiki ya Sheria ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa: nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jin
ai"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa