Na Kitengo cha Mawasiliano
Wanawake kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara wameadhimisha siku yao kwa kitembelea na kutoa msaada wa Vyakula katika Shule ya Msingi Mji Mpya maalumu iliyopo Halmashauri ya Wilaya Tandahimba
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao Mkaguzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Dafroza Justinian amesema wameamua kuadhimisha Siku hiyo katika Shule hii ili kuwa sehemu ya familia na kufurahi pamoja.
"Tuwapende hawa watoto, tumetoa kidogo tulicho nacho lakini mioyo yetu imefarijika na kufurahi pamoja nao katika siku yetu hii muhimu" Dafroza
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri amewashukuru kwa Msaada walioutoa , kuthamini na kuchagua kuadhimisha siku hiyo katika Wilaya ya Tandahimba.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Mkoa wa Mtwara yamefanyika Wilaya ya Masasi ambapo Wilaya ya Tandahimba imeshiriki.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa