Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa pamoja na Kamati ya Usalama (KU) Wilaya wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maji ,Kituo cha Afya Litehu pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kubangua Korosho Kitama
Ziara hiyo imefanyika leo Septemba 15,2022 ambapo KU ilianza kwa kutembelea chanzo cha maji cha Mitema kasha mradi wa maji Mkwiti ili kuona shughuli zinazoendelea ikiwa pamoja na matanki ya kuhifadhia maji
Wakiwa katika Kituo Cha Afya Litehu walikagua ujenzi wa jengo la kufulia na jengo la upasuaji mama na mtoto ambao unatekelezwa kwa fedha Kutoka Serikali Kuu kiasi cha Shilingi Mil.250 na kuridhishwa na maendeleo ya majengo hayo
Dc Sawala akiwa katika mradi wa maji Mkwiti alisikiliza kero za wananchi wa mangombya kuhusu kukosa maji kwa muda wa wiki tatu Ambato alitoa ufafanuzi kuwa kuna matengenezo ya mambomba yanaendelea katika chanzo cha maji Mitema lakini aliagiza wataalam kufungulia maji yaliyopokatika tanki la Mkwiti ili wananchi waweze kupata huduma hiyo huku wakisubiri matengenezo yakamilike
“Poleni kwa kukosa maji kuna matengenezo katika chanzo cha maji Mitema unaendelea tumefika huko na tumeona kazi inaendelea,kwa sasa wataalamu nimewaagiza wafungue maji yaliyopo katika tanki ili watanzania mpate maji,nawasistiza wataalam kuwapa taarifa wananchi endapo kuna matengenezo mnafanya kupitia viongozi wao wa vijiji,wao hawawezi kujua kinachoendelea bila kuambiwa,”amesema Dc Sawala
Aidha wakiwa katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho Dc amempongeza mwekezaji ambaye ni mzawa kwa kuwekeza Tandahimba ujenzi wa kiwanda hicho chenye thamani ya shilingi Bil.2.5 ambacho kitatoa fursa kwa wananchi kupata ajira
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa