*Klabu za lishe Shuleni zatiliwa mkazo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti ameongoza Kikao Cha utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa afua za lishe Cha Robo ya Tatu Januari-Machi 2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Awali akifungua Kikao hicho Mkuti amewasisitiza watendaji wa Kata kufuatilia suala la lishe na usimamizi Mzuri wa klabu za lishe Shuleni ili wanafunzi waweze kupata lishe Bora na kujenga Jamii yenye Afya.
"Fatilieni suala la klabu za lishe Shuleni, suala hili ni la umuhimu,kila mmoja akaongee na Mkuu wa Shule,ili tuhakikishe walimu wahakikishe wanapata chakula chuleni,Mhe.Rais anasisitiza sana suala hili nasi tulichukulie kwa uzito" Mkuti.
Aidha, akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mkataba huo Afisa Lishe Wilaya ya Tandahimba Asha Selemani amesema Kata ya Luagala imeongoza kwa kupata 97% katika utekelezaji wa Viashiria vya Mkataba wa lishe kati ya Kata 32 na kupongezwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya .
#Kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa