Na Kitengo cha Mawasiliano
Watendaji Kata Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamesistizwa kuendelea kusimamia afua za lishe kwenye maeneo yao kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa ili kuwa na Jamii yenye afya bora.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndugu Francis Mkuti kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mikataba wa lishe ngazi ya Kata kwa kipindi cha Robo ya Pili Mwaka 2023/2024 Januari 30,2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri,amesema kuwa Jamii ikiwa na afya njema na shughuli za Maendeleo zinafanyika kwa ufanisi
" Mkafanye ufuatiliaji endelevu wa masuala ya afua za lishe kwenye maeneo yenu katika kuhakikisha afya za watoto zinaimarika kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa,lakini pia hakikisheni mnakuwa na takwimu sahihi za lishe kwenye maeneo yenu," amesema Mkuti.
Akiwasilisha taarifa yake Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu.Asha Selemani amesema kwa kipindi cha robo ya pili upatikanaji wa chakula mashuleni haukuwa wa kuridhisha kwa baadhi ya Kata .
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dkt.Grace Paul amewapongeza Watendaji Kata kwa kuendelea kutekeleza afua za lishe kwenye maeneo yao huku akiwasistiza kuendelea kushirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii ili wajawazito waliopo Kwenye maeneo yao wajifungulie kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa