Na Kitengo cha Mawasiliano.
Kikao cha tathimini ya utekelezaji afua za lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kimefanyika ambapo Wamejadili utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Kata.
Akisoma taarifa ya robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 Novemba 10,2023 Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Asha Selemani amesema kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na utoaji wa Elimu ya unasihi kwa walengwa,Maadhimisho ya Siku ya afya na Lishe ya kjiji kwa Kata zote 32 ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika na Upatikanaji wa Chakula kwa Wanafunzi kwa Shule zote za Msingi na Sekondari.
Kwa upande wake Ndg.Boni Minga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba amewapongeza Watendaji wa Kata kwa kutekeleza afua za lishe kwenye maeneo yao ambapo amewasistiza kuendelea kutekeleza viashiria vya Mkataba wa Lishe ili Jamii iendelee kuwa na afya bora.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa