Na Kitengo cha Mawasiliano
Kiasi cha Shilingi Milioni 70 za Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zimetumika kutengeneza madawati 1000 ya wanafunzi wa Shule za Msingi
Akikabidhi madawati 300 ya awamu ya kwanza kwa shule kumi za Msingi Nov 2,2022 Mhe.Mohamed Namgugu Diwani wa Kata ya Mahuta ambapo amekabidhi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kuwa madawati yao ni moja ya faida za uchangiaji wa mfuko wa Elimu wa Halmsahauri
“Mfuko huu wachangiaji wakubwa ni Wakulima wa Tandahimba kwaiyo leo tunakabidhi madawati haya 300 kwa shule za Msingi ili wanafunzi wetu wakae huku mengine yakimaliziwa,Mfuko huu unatusaidia wanatandahimba tuendelee kuchanhia mfuko huu ili uzidi kufanya vitu vikubwa katika kuboresha Elimu ndani ya Wil,aya yetu,”amesema Mhe.Namgugu
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi Ndg Samwel Mshana akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ametoa wito kwa Walimu Wakuu kuyatunza madawati hayo ili yaweze kuwasaidia wanafunzi
Aidha Naye Mwl.Shamsia Mohamed akizungumza kwa niaba ya Walimu Wakuu wengine ambao wamekabidhiwa madawati hayo wameshukuru na kuupongeza hatua hiyo ambapo amebaisha kuwa madawati hayo yatapunguza changamoto ya madawati katika shule zao
Hata hivyo Ndg.Dadi Dadi Mkazi wa Mahuta amepongeza hatua hiyo na kutoa rai kwa wakulima na wanachi wa Tandahimba kuendelea kuchangia mfuko wa Elimu ili uweze kuleta maboresho katika Elimu ndani ya Wilaya ya Tandahimba
Shule za Msingi ambazo zimepokea madawati hayo ni Nanhyanga A,Nanhyanga B,Namkomolela,Mndumbwe,Mahuta Bondeni,Majengo,Mkonjowano,Nachunyu,Malamba na Mkulung’ulu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa