Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amepokea fedha kiasi cha shilingi Bil. 1.76 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa vyumba vya madarasa 88
Mkurugenzi Mtendaji ndg Mussa Gama taarifa ya jinsi ya kutekeleza miradi hiyo kwa wakati
Fedha hizo za Mpango wa Maendeleo ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 zimetolewa na Serikali kuu ili kuboresha sekta ya Elimu katika Wilaya ya Tandahimba naTanzania kwa Ujumla
Fedha hiyo itatekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa 82 kwa shule za sekondari na vyumba vya madarasa shikiziki 6 kwa shule za Msingi tatu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo kila darasa moja litakamilika kwa gharama ya shilingi Mil.20
Mkurugenzi Mtendaji Ndg Gama akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wasimamizi wa miradi ya madarasa 88 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Mkurugenzi amefanya kikao kazi na wasimamizi wa miradi hiyo ili kuhakikisha miradi inakamalika kwa wakati lakini pia kwa kutumia njia ya ‘Force Account’ kwa usahihi ili madarasa hayo ifikapo January 2022 wanafunzi wa kidato cha kwanza waweze kutumia
Wasimamizi wa miradi ya vyumba vya madara wakiwa kwenye kikao kazi
Aidha hatua ya uchimbaji wa misingi katika maeneo ambayo miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa itatekelezwa inaendelea ndani ya Halmashauri ya Tandahimba i
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa