Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kiasi cha Shilingi 213,100,000 kimetumika kwenye malipo ya walengwa 6175 wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wilaya ya Tandahimba kati ya walengwa 6225 huku kiasi cha shilingi 1,472,000 kimebaki baada ya walengwa 50 kutoshiriki kwenye zoezi hilo kwa sababu mbalimbali
Hayo yamebainishwa kwenye taarifa ya tathimini ya zoezi la malipo na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi ambapo amesema malipo ya mwezi wa 3 na 4 yamefanyika kwa siku tano mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu katika maeneo husika
Malipo hayo yamefanyika kwa vijiji 88 ambavyo vipo kwenye mpango Wilayani Tandahimba ambapo wawezeshaji wa malipo walizingatia kanuni na sheria katika kuendesha zoezi la malipo kwenye vijiji
“Kaya 50 ambazo hazijashiriki malipo zilikuwa na sababu mbambali ikiwemo vifo,walengwa kutokuwepo kwenye maeneo yao wakati wa malipo na walengwa wengine wamefuzu na kujiondoa kwenye mpango,lakini kwa ujumla zoezi limemalizika vizuri”amesema Mratibu
Aidha amesema kuwa miongoni mwa changamoto ambazo zimejitokeza katika zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya walengwa kutokuwa na vitambulisho na walengwa wengine majina yao kutoonekana katika orodha ya malipo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa