Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mfuko wa Maendeleo ya Jamiii (TASAF) Halmashauri ya Tandahimba umefanikiwa kuhakiki Kaya maskini 5758 katika zoezi la uhakiki wa kipindi cha pili awamu ya tatu ambazo zitaendelea na mpango wa malipo kati ya kaya 6873 zilizokuwepo awali
Kaya ambazo zilifika katika zoezi la uhakiki kwenye vituo mbalimbali ni Kaya 6271 na Kaya 604 hazikuweza kufika kwenye uhakiki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuwa nje ya maeneo yao kwa shughuli mbalimbali
Walengwa wakisubiri kuhakikiwa katika zoezi hilo
Mratibu wa TASAF Halmashari ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi amesema kuwa kati ya Kaya 6271 ambazo zimehakikiwa kaya 313 zimeondolewa kwenye mpango wa malipo baada ya kupoteza sifa za kuendelea
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi
“Ambao hawakufanyiwa uhakiki hawataweza kuingizwa kwenye mpango wa malipo mwezi Julai na Agosti lakini zoezi limeenda vizuri kwa wakati uliopangwa na uhakiki umefanyika kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na tumefanikiwa katika hilo,”amesema Mbilinyi
Baadhi ya changamoto ambazo zimejitokeza katika zoezi la uhakiki wa kipindi cha Pili awamu ya tatu ni pamoja na muda kuwa mdogo hivyo baadhi ya walengwa kutofanyiwa uhakiki
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa