Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara ndugu Mgeni Haji ameridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ilani ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tandahimba
Ameyasema hayo Novemba 30,2021 kwenye ziara yake ya kujitambulisha kwenye Chama na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ilani ya CCM ukiwemo mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na vituo vya afya
“Nimetembelea miradi ya vyumba vya madarasa na kituo cha afya mambamba nimeona mpo hatua nzuri,lakini pia kwenye taarifa ya Mheshimiwa Dc amesema kuwa mnashirikiana vizuri katika kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele Tandahimba,nawapongeza sana ushirikiano na umoja mliokuwa nao,”amesema Katibu
Aidha ametoa agizo kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanafanya mkutano na wananchi kuwashirikisha fedha ambayo itabaki baada ya mradi kukamilika ili waweze kupanga matumizi pamoja
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa miradi hiyo imeweza kufika hatua nzuri kwasababu kila mmoja amewajibika kwa nafasi yake ili miradi ikamilike kwa wakati
“Katika kusimamia miradi hii kila mmoja anawajibika katika eneo alke Madiwani,Mkurugenzi Mtendaji Wakuu wa Idara na wasimamizi wa maeneo ya mradi wote wanashiriki kuhakikisha tunamaliza kwa wakati,”amesema Dc Sawala
Katika majumuisho ya ziara hiyo katibu amesistiza ushirikianao uendelee kuimarika kati ya Madiwani, wataalam,ofisi ya Mkurugenzi,Ofisi ya Dc na Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza miradi ya maendeleo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa