Na Kitengo cha Mawasiliano
Wananchi wote mnakaribishwa katika Maonesho ya Nane Nane ambayo kwa Kanda ya Kusini yanafanyika Ngongo-Lindi.
Katika Banda la Tandahimba bidhaa mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonyeshwa sambamba na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wanaendelea kutoa Elimu ya bidhaa na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Banda hilo.
Aidha, katika Banda la Tandahimba Kuna ushauri wa kiafya juu ya lishe Bora , baadhi ya vipimo vinatolewa sambamba na kupima Uzito.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Nane nane 2024 inasema "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa