Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele ameongoza kikao Cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya(DCC) Kwa ajili ya kupitia na kujadili makisio ya Bajeti ya Halmashauri ya Tandahimba kwa Mwaka 2025/2026 .
Katika Kikao hicho Kanali Mntenjele amesisitiza Ofisi ya Mkurugenzi kuzingatia Ushauri uliotolewa na kamati hiyo wenye lengo la kujenga kwa kufanya marekebisho ili Bajeti iwe na tija kwa Wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imewasilisha makadirio ya Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 inayofikia Tsh.Bilioni 40.2 ikijumuisha Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi, Ruzuku ya Mishahara, Matumizi Mengineyo(OC) na Mapato ya n
dani.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa