Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Katika kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho Halmashauri ya Tandahimba na Chama kikuu cha ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu) wamekabidhi misumeno(chain saw) 14 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 25 kwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba (kushoto) akimkabidhi mashine Afisa Tarafa ya Namikupa Boni Minga(Kati)
Akikabidhi misumeno hiyo kwa maafisa Tarafa Dc Waryuba amesema kuwa misumeno hiyo ikatumiwe kama ilivyokusudiwa ili iweze kuleta mafanikio katika kampeni ya ondoa mapori ongeza uzalishaji ambayo imeanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa
“Misumeno hii tunaigawa kwa tarafa zote saba ikatumike ilivyokusudiwa tusisikie inafanya kazi tofauti nia yetu tuongeze uzalishaji katika Wilaya yetu,kuna mikorosho ina miaka zaidi ya miaka 70 imepunguza uzaliashaji,”amesema Dc Waryuba
Dc Waryuba akikabidhi mashine kwa Afisa Tarafa wa Mchichira Doto Nyirenda
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Said Msomoka amesema Halmashauri imenunua misumeno 7 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12 ili kuongeza uzalishaji ili wakukuza pato la wananchi na kuongeza mapato yatokanayo na zao hili
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka(kushoto) akimkabidhi mashine7 za chain saw Dc Waryuba(kulia)
“Tumekabidhi mashine hizi ili kuunga mkono kampeni ya Ondoa mapori ongeza uzalishaji ili wananchi waongeze uzalishaji waongeze kipato na sisi tupate mapato,”amesema Ndugu Msomoka
Aidha Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu)Mohamed Nassoro amesema kuwa wametambua umuhimu wa kampeni hiyo kwa wakulima ili kukuza uzalishaji wa zao la korosho
Mwenyekiti wa Tanecu akikabidhi mashine 7 kwa Dc Waryuba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa