Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele amezindua kampeni ya chanjo ya Mifugo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tandahimba akiwasisitiza Maafisa Ugani kuhakikisha wanatoa Elimu ya chanjo kwa Wananchi hasa Wafugaji ili waweze kuchanja mifugo yao na kuilinda dhidi ya magonjwa.
Aidha, DC Mntenjele amewaasa Maafisa Ugani wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatekeleza Majukumu yao kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi .
"Kila mmoja atekeleze Majukumu yake kwa kuzingatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Mifugo, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Mifugo, Sheria ya wanyama na kanuni mbalimbali zilizopo ili kupata matokeo chanya ya zoezi hili kwa kuwa Serikali inatoa fedha nyingi Kwa ajili ya Chanjo ya Mifugo kila Mwaka" DC Mntenjele
Awali akizungumza hafla hiyo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba David Sinyanya amesema kupitia Maafisa Ugani wanatarajia zoezi la chanjo kufanyika kwa ufanisi.
Kwa upande wake Afisa Mifugo Wilaya ya Tandahimba Mtaalam Mkana amesema zoezi la kuchanja Mifugo litaanza Februari 26 hadi Aprili 29 2025 wakitarajia kuchanja zaidi ya Mifugo 180,000 Wakiwemo Ng'ombe, Mbuzi,Kondoo na Kuku.
Maafisa ugani kilimo na maafisa ugani mifugo wa kata, vijiji na wa ngazi ya Wilaya pamoja na baadhi ya Wafugaji wamehudhiria katika Uzi
nduzi huo.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa