Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Tandahimba(KU) ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala wametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya afya vitano vyenye Jumla ya gharama ya shilingi Bil. 2.3
Ziara hiyo imefanyika Mei 25,2023 ambapo miradi minne ya vituo vya afya imetekelezwa kwa kiasi cha shilingi 1,900,000,000 fedha kutoka Serikali Kuu na kimoja kimetekelezwa kwa kiasi cha shilingi 400,000,000 fedha ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri na kufanya Jumla ya miradi ya ujenzi wa vituo vya afya vitano kuwa shilingi 2,300,000,000 (Shilingi Bilioni mbili na Milioni mia tatu)
Miradi ya Ujenzi wa Vituo vya afya vilivyotembelewa ni kituo cha Afya KitamaTsh. 400,000,000,ujenzi wa kituo cha afya Mambamba Tsh.500,000,000.,ujenzi wa kituo cha afya Mihambwe Tsh.500,000,000,ujenzi wa kituo cha afya Maheha Tsh.400,000,000 na Ujenzi wa kituo cha afya Litehu Tsh.500,000,000
Dc Sawala akiwa katika ziara hiyo kuona hali halisi ya vituo hivyo amesistiza vituo hivyo kuanza kutoa huduma kwa wananchi " Nasistiza vituo hivi vianze kufanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji ulivyoahidi kuwa vitaanza rasmi mwanzoni mwezi Juni na vingine Julai, 2023 hilo lisimamiwe ili wananchi wapate huduma katika vituo hivi," amesema Dc Sawala
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa