Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tandahimba imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ilani ya CCM ndani ya Wilaya
Akizungumza Desemba 17,2021 wakati akikagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ndugu Omary Nang’uta ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia miradi hiyo lakini ameagiza kasoro ndogo ndogo ambazo zimebainika kwa baadhi ya miradi zirekebishwe
“Tunashukuru kwa jinsi mnavyoisimamia ilani ya CCM tumeridhika na miradi hii lakini zipo kasoro ndogo ndogo ambazo tumeziona kwa baadhi ya miradi mziweke sawa,lakini wa ujumla tunaishukuru Serikali kwa miradi ya vyumba vya madarasa,vituo vya afya na barabara ambayo wananchi wa Tandahimba tutanufaika nayo ,”amesema Mwenyekiti
Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu shule shikizi Mpikula ambayo ilitembelewa na kamati ya siasa Wilaya
Aidha kwa upande wa barabara inayoendelea kujengwa ya kilomita 2.15 Kamati ya siasa imeshauri kuweka utaratibu mzuri ilikuweka barabara mbadala na kuzuia maji kutwama kuepuka adha kwa wananchi hasa katika kipindi cha masika
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amesema kuwa kasoro hizo ambazo zimebainika zitafanyiwa kazi ili miradi hiyo iweze kuwa bora zaidi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa