Na Kitengo cha Mawasiliano.
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tandahimba ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe. Ismaili Mkadimba imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Ziara hiyo imefanyika leo Novemba 29,2023 ambapo Kamati imetembelea chanzo cha Maji Mitema na kuona kazi zilizopangwa kufanyika kuongeza uzalishaji wa maji ili wananchi wa Tandahimba waendelee kunufaika na chanzo hicho,Mradi wa maji Mkwiti unaotekelezwa na RUWASA na Mradi wa Maji wa Miji 28 wenye gharama ya Tsh.Bil 84.7 unaotekelezwa na Makonde.
Aidha Mwenyekiti wa CCM Mhe.Mkadimba ameagiza kuongeza kasi na usimamizi katika utekelezaji wa mradi wa Mkwiti uweze kukamilika ili urahisishe upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa vijiji 17 ambavyo vina jumla ya wakazi 26,164.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba Injinia Antidius Muchunguzi akiwasilisha taarifa yake ya mradi wa maji Mkwiti amesema utekelezaji unaendelea ambapo kazi zingine zilizopangwa kufanyika zimekamilika.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa