Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tandahimba Mhe.Ismaili Mkadimba.amewataka wasimamizi wa Miradi kuongeza Juhudi katika kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo ili wananchi wapate huduma ambazo Serikali imekusudia kwa wakati.
ameyasema hayo Leo Oktoba 3, 2023 wakati Kamati ya Siasa Wilaya ya Tandahimba ilipofanya ziara ya ukaguzi wa Miradi mbambali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Aidha, kamati ya Siasa Wilaya imeishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa Fedha za Miradi katika Sekta za Afya, Elimu, Barabara, Maji na Nyinginezo ambapo kwa Pamoja zinalenga kuwahudumia na kuleta chachu ya Maendeleo kwa Wananchi wa Tandahimba.
Jumla ya Miradi yenye thamani ya zaidi ya Tsh.Bilioni 7.5 imekaguliwa na Kamati hiyo ukiwemo Mradi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Amani, Mabweni Mawili Shule za Sekondari Kitama na Luagala, Miradi ya Maji Kitama na Mkwiti, Pamoja Nyumba ya Mwaalimu (2-1) Shule ya Sekondari Litehu ,Ujenzi wa Zahanati Nachunyu pamoja na Machinjio ya Halmashauri.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa