Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Said Nyengedi imekagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kitama na kupongeza utekelezaji wa mradi huo ambao umeanza kutoa huduma kwa wananchi
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 3,2023 na Kamati ya Siasa Mkoa ambayo imetembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kitama ambao umetekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri
"Nawapongeza kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM lakini kwa Ushirikiano mlionao ambapo umefanikisha utekelezaji wa mradi huu kukamilika na wananchi wameanza kupata huduma za afya ," amesema Mhe.Nyengedi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ameshukuru juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Tandahimba
Mradi wa Kituo cha Afya Kitama umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Mil.400.6 ikiwa mapato ya ndani ambapo imejenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) nyumba ya mganga,kichomea taka na Jengo la wazazi na Upasuaji
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa