Na Kitengo cha Mawasailiano
Ikiwa ni siku moja tangu kuanza kwa zoezi la Sensa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ameongoza kikao cha Kamati ya Sensa Wilaya kufanya tathimini ya Zoezi la Sensa linavyoendelea
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa DC Agosti 24,2022 Dc Sawala amesema kuwa zoezi limeanza vizuri hakuna changamoto kubwa ambazo zimejitokeza kwa siku ya kwanza
Katika kikao hicho ametoa wito kwa wenyeviti wa vitongoji kutoa taarifa kwa wananchi wa maeneo yao utaratibu wa karani kupita katika kaya ili wananchi waweze kuendelea na majukumu mengine ya kiuchumi
“Nitoe wito kwa wenyeviti wa vitongoji kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wananchi kuwa karani atapita lini katika kaya yake ili aweze kuendelea na majukumu mengine ya kiuchumi kuliko akae kusubiri kuhesabiwa wakati hajui karani atapia lini,njia hii itasaidia wananchi kuendelea na majukumu mengine,”amesema Dc Sawala
Zoezi la Sensa linaendelea katika Halmsahauri ya Wilaya ya Tandahimba huku wananchi wakiwa na hamasa ya kuhesabiwa kwa ajili ya Maendeleo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa