Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala akihamasisha wananchi kushiriki sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022
Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Sensa Wilaya ya Tandahimba ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mhe.Kanali Patrick Sawala wameanza ziara ya kutembelea kata zote 32 zilizopo Halmashaiuri ya Wilaya ya Tandahimba kuhamasisha Wananchi kuhesabiwa Agosti 23,2022
Ziara hiyo ya siku tatu imeanza Agosti 11-13 ,2022 ambapo katika kamati hiyo zimegawanyika katika timu tatu ambazo zitatembelea katika kila kata kuhamasisha Sensa
Akizungumza na Wananchi Dc Sawala amewasistiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa ili kupata takwimu sahihi amzazo zitasaidia katika Mipango ya Maendeleo kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Taifa
"Nawasitiza wananchi kushiriki kluhesabiwa Agosti 23,2022,usikubali mtu akupotoshe ili usihesabiwe,lengo la sensa ni njema,na siku hiyo kila mtu atahesabiwa mara moja tu hata kama ana familia tatu au nne,lengo ni kupata taaarifa sahihi,"amesema Dc Sawala
Aidha amehimiza kamati za Sensa kuanzia ngazi ya Vitongoji hadi Kata kuendelea kutoa hamasa katika maeneo yao sambamba na kubainisha maeneo ambayo ufikaji wa makarani ni changamoto ili utaratibu ufanyike mapema ili kila mwananchi ahesabiwe tarehe hiyo
Katika ziara hiyo ya utoaji wa Elimu na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ambayo Agosti 11,2022 Kata 11 zimefikiwa kwa siku ya kwanza ambazo ni Mihambwe,Mkoreha,Naputa,Namikupa,Mchichira,Mnyawa,Lukokoda,Mkundi,Nambahu,Mkonjowano na Litehu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa