Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Tandahimba (WDC) ikiongozwa na DIwani wa Kata hiyo Mhe.Adinani Chipande imekabidhi mahindi tani moja na nusu yenye gharama ya Tsh. 1,350,000 kwa shule tano za msingi zilizopo Kata ya Tandahimba Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ili kuamsha ari kwa wazazi kuchangia upatikanaji wa chakula shuleni
Akikabidhi mahindi hayo kwa Walimu Wakuu wa Shule ya Msingi Nandonde,Amani,Mjimpya,Matogoro na Madaba leo Juni 3,2023 katika Ofisi ya Mtendaji Kata ya Tandahimba Mhe.Chipande amesema kuwa pamoja na kuhamasisha wazazi na walezi kuchangia WDC imechukua hatua hiyo ili upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi ufikie asilimia 100kwa shule za msingi na sekondari katika kata hiyo
"Mahindi haya nakabidhi kwa shule zetu tano za msingi ili wanafunzi wakifungulia shule waweze kupata chakula,tumeanza leo lakini tutaongeza mahindi mengine kila shule itapata KG 500 ambapo shule yetu ya Sekondari Nandonde nayo itapata," amesema Diwani
Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Tandahimba Mwl.Salum Mohamed ameipongeza WDC kwa kuzipatia mahindi shule hizo ambapo pia ametoa wito kwa wazazi kuchangia upatikanaji wa chakula shuleni ili wanafuzi wote wapate chakula
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nandonde Mwl. Salha Mnango kwa niaba ya Walimu Wakuu wa shule zilizopokea mahindi hayo ameishukuru WDC na kueleza kuwa chakula ni muhimu kwa ustawi wa wanafunzi hivyo watayahifadhi ili wanafunzi wakifungua shule waweze kupata chakula
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa