Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Maafa Wilaya ya Tandahimba imetakiwa kuandaa Mpango wa Wilaya wa dharura ili kukabiliana na Maafa yanapotokea
Hayo yamesemwa na Mwezeshaji Bi.Winfrida Ngowi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa katika kikao kazi cha siku mbili kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Agosti 16-17,2022
Amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kutoa elimu kuhusu dhana ya majanga na maafa, kuchanganua hali ya maafa kwa sasa katika Wilaya ya Tandahimba na kujiwekea mpango wa kuweza kukabiliana dhidi ya majanga na maafa yanapotokea
Akifungua mafunzo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa mafunzo hayo yatawezesha Kamati ya Wilaya kujiwekea Mpango madhubuti ambao utasaidia kukabiliana na maafa lakini pia kudhibiti majanga
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Wakuu wa Idara na Vitengo,Kamati ya Ulinzi na Usalama,Taasisi za serikali,viongozi wa dini na watu maarufu wameweza kupata uelewa wa jinsi ya kukabiliana na majanga ambayo yanasababisha maafa ili kupunguza athari
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa