Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Baisa Baisa amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri
Mhandis Hassan Msangawenga akionyesha ujenzi wa mradi wa vyumba viwili vya madarasa Sekondari ya Nandonde
Ameyasema hayo kwenye ziara ya Kamati ya Fedha ,Utawala na Mipango walipotembelea miradi ya maendelo inayoendelea na iliyokamilika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Tandahimba
Kamati ya Fedha wakiangalia mradi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Kitama moja
“Tumetembelea miradi kujionea hali halisi tumeiona miradi ipo imekamilika vizuri na mingine ina changamoto lakinipia naiomba jamii kujitolea kushiriki kwenye sisi wana Tandahimba miradi ni yetu ,tushiriki kikamilifu serikali inatoa fedha lakini tusipoongeza nguvu tutakwama”,amesema Mh Baisa
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Likapa Nangololo (kushoto)akiangalia mradi wa kisima cha kuhifadhia maji katika zahanati ya Namikupa
Aidha amesema kuwa kuna baadhi ya miradi inahitilafu ndogo ndogo lakini kwakuwa Mhandisi wa Wilaya ameiona ataishughulikia ili iwe imara zaidi wananchi waendelee kutumia na kuleta manufaa kwa jamii
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya fedha wakimsikiliza msimamizi wa mradi wa matundu vyoo Zahanati ya Namikupa
Naye Mhandisi wa Ujenzi Hassani Msangawenga amesema kuwa miradi ambayo imeonekana na changamoto zitarekebishwa na itakuwa vizuri “Mapungufu ambayo yameonekana kwa mradi baadhi ya miradi tutasimamia na kurekebisha kwakuwa uwezekano upo,”amesema Mhandisi
Mhandisi Hassan Msangawenga akitoa maelezo ya mradi kwa kamati ya fedha
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa