Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya fedha,Utawala na Mipango ya Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba imetembelea miradi ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba za walimu,ujenzi wa matundu ya vyoo na umaliziaji wa vyumba vya madarasa inayotekelezwa katika shule za msingi
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa akiwa pamoja na Timu ya Menejimenti (CMT) Februari 1,2023 ambapo amesistiza kasi katika ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kuzingatia mpango kazi wa mradi husika
“Tunamshukuru Rais wa Awamu ya sita Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika shule zetu za msingi,mafundi viongozi hakikisheni miradi inakamilika kwa wakati ili iweze kutumika,”amesema Mhe.Baisa
Miradi iliyotembelewa ni umaliziaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya msingi Malamba,Umaliziaji wa ujenzi wa chumba kimoja shule ya msingi Nahnyanga A,umaliziaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Msingi Nahnyanga B
Aidha miradi mingine ni ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Machedi kata ya Mkwedu,ujenzi wa matundu 10 ya vyoo na nyumba ya mwalimu shule shikizi Amani kata ya Chaume na ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Mnaida kata ya Nambahu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa