Na Kitengo cha Mawasiliano
Kamati ya Fedha Utawala na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa pamoja na Wataalamu (CMT) imetembelea kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Kamati ya fedha ikikagua miradi ya maendeleo
Miradi ambayo imetembelewa na Kamati hiyo Julai 28,2022 ni Uendelezaji wa Zahanati ya Mitumbati iliyopo kata ya Kwanyama,Ujenzi wa mradi wa chumba cha darasa shule ya msingi Namdowola kata ya Nanhyanga,Ujenzi wa chumba kimoja Sekondari ya Chaume,Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mndumbwe,ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya msingi Mkwiti
Mradi wa chumba kimoja cha darasa shule ya msingi Namdowola
Aidha wametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Namindondi iliyopo kata ya Ngunja,Ujenzi wa kituo cha afya Litehu,Ujenzi wa sekondari ya Litehu, Ukarabati wa wodi ya wajawazito zahanati ya kata Mkonjowano na umaliziaji wa maabara ya sayansi shule ya sekondari Lyenje
Wataalamu wakisikiliza taarifa ya mradi kutoka kwa msimamizi wa mradi wa kituo cha afya Litehu (hayupo pichani)
Jengo la kufulia kituo cha afya litehu
Akizungumzia ziara hiyo Mwenyekiti Mhe.Baisa amesema kuwa mipango kazi izingatiwe katika miradi ili iweze kukamilika kwa wakati , ubora unaotakiwa pia thamani ya fedha ionekane katika mradi husika
Mwenyekiti Mhe.Baisa akisistiza jambo eneo la mradi
Baadhi ya vyumba vya madarasa Sekondari ya Litehu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa