Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Januari 24, 2024 imefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo ikiwemo Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji , Madarasa Mawili , Ofisi na Matundu 8 ya Vyoo katika Shule Shikizi za Mihambwe na Michenjele wakisisitiza Kasi iongezeke .
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Baisa Baisa amesema pamoja na kuwa Miradi inaendelea vizuri ametahadharisha wasimamizi kuepuka kuwalipa wazabuni kabla hawajamaliza kazi ili kuepuka ucheleweshwaji wa Miradi kukamilika.
"Walimu mnaoidhinisha Malipo msiingie kwenye Mtego, msiwalipe wazabuni kama kazi haijafanyika" Mhe.Baisa.
Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inayojengwa kwa Gharama ya Tsh Milioni 180 inatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 15, 2024 huku Shule shikizi za Mihambwe na Michenjele zenye Gharama ya Tsh.Milioni 54 kila Moja zinatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 28, 2024.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa