Na Kitengo cha Mawasiliano.
Kamati ya Fedha Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Novemba 9, 2023 imekagua Miradi 10 ya Maendeleo katika Sekta ya Afya, Elimu na Uvuvi yenye Jumla ya Tsh.Bilioni 1.1 inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Baisa Baisa amesema Serikali inatoa Fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo hivyo ni jukumu la Viongozi na watumiaji wa Miradi hiyo kuitunza ili idumu kwa Muda mrefu.
Aidha, Mhe.Baisa amesisitiza Wakandarasi walipwe kulingana na kazi wanazozifanya ili kuongeza Kasi na utendaji wa kazi Kwa makini zaidi ikilinganishwa na wanapopewa Fedha kiasi kabla ya Mradi kukamilika.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Mnyawa ambae ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya Fedha Mhe. Rashid Njawala amesisitiza maelekezo ya kuboresha yanayotolewa na Kamati yafanyiwe kazi ili watakapokagua mara nyingine wakute miradi ikiwa katika Ubora zaidi.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Robert Mwanawima ameahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Kamati yenye lengo la kuboresha miradi hiyo huku akisisitiza kuendelea kufanya ufuatiliaji kupitia Menejimenti ya wataalamu katika kutekeleza Miradi hiyo kwa ufanisi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa