Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ACI.Mariam Mwanzalima amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuimarisha ushirikiano ili kuwahudumia wananchi katika maeneo yao kwa ufanisi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Kata ya Michenjele na Mihambwe kwa nyakati tofauti Oktoba 23,2023.
"Mkishirikiana nyie viongozi kuanzia ngazi ya Vijiji hadi Kata mtafika mbali kwakuwa mtaweka mikakati mizuri ya Maendeleo kwenye Kata yenu hususan ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya vijiji na kuwawezesha wananchi kiuchumi hususan vijana," amesema ACI.Mwanzalima.
Aidha amewasistiza viongozi kufanya vikao katika maeneo yao sambamba na kutoa elimu kwa jamii kwenye Mikutano ili waweze kuunda vikundi vya uzalishaji Mali na kuibua fursa zilizopo katika maeneo yao.
Mkurugenzi Mtendaji ACI.Mwanzalima Oktoba 23,2023 amefanya ziara ya kutembelea Kata Michenjele na Mihambwe na kuzungumza na Viongozi wa Kata wakiongozwa na Diwani wa eneo husika na Wenyeviti wa Vijiji ambapo pia amesikiliza changamoto zinazowabili na kuzitatua.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa