Na Kitengo cha Mawasiliano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Mariam Mwanzalima kuwachukulia hatua za kisheria watumishi watakaohusika kuhujumu pembejeo za wakulima
Amesema hayo leo Agosti 23,2023 katika Mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani robo ya nne 2022/2023 uliofanyikakwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na madiwani,wataalamu,viongozi wa vyama vya siasa na wananchi
" Wapo baadhi ya wananchi hawajapata pembejeo katika Kata zetu kutokana na baadhi ya watu ambao siyo waadilifu,Mkurugenzi chukua hatua kwa upande wa watumishi ambao watabainika kuhusika katika suala la kuhujumu pembejeo za wakulima," amesema Mhe.Baisa
Aidha amemsistiza Mkurugenzi kuhakikisha watendaji wanaishi katika maeneo yao ya kazi huku akitoa wito kwa madiwani kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao
Naye Ndg.Mtaalam Mkana akifafanua suala la pembejeo kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Mifugo Kilimo na Uvuvi amesema kuwa utaratibu umewekwa katika awamu ya pili ya ugawaji wa pembejeo ili wakulima wapate pembejeo stahiki ambapo amesistiza kila mkulima kuchukua pembejeo kwenye amcos ya kijiji chake
Kwa upande wa madiwani wamepongeza taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji iliyowasilishwa katika baraza hilo na kumuahidi kumpa ushirikiano ili Tandahimba isonge mbele
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa