Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetumia shilingi Milioni 62 kununua vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kujinga na maambukizi ya Covid -19
Vifaa hivyo vimenunuliwa kwa fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na vimekabidhiwa kwa Hospital ya Wilaya ya Tandahimba
Dc Waryuba (Kulia) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai
Akikabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kuwa vifaa hivi vitakuwa msaada ndani ya Wilaya lakini pia ni jukumu la wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujinga na ugonjwa wa virusi vya korona
Dc Waryuba (Kulia) akielezea jambo (Kati)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka(Kushoto) Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai
“Nakabidhi vifaa hivi ambavyo vimenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani ili kupambana na maambukizi ya korona bado naendelea kuwasistiza wananchi waendelee kujikinga kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ,kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni pamoja na kufuata maagizo yanayotolewa na wataalamu wetu wa Wizara ya afya ,”amesema Waryuba
Naye Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai ameshukuru Halmashauri kwa jitihada ambazo wamezichukua kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo ni msaada katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona
Mganga Mkuu wa Hospitali Dk Antpas Swai (kushoto) akitoa shukrani baada ya kupokea vifaa hivyo
“Nachukua nafasi hii kushukuru Halmashauri kwa kutuletea vifaa tiba hivi kwa ajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona ndani ya Wilaya yetu,”amesema Dk. Swai
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa