Na Kitengo cha Mawasiliano.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba leo Machi 5,2024 imezindua Programu Jumuishi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto ili kuhakikisha mtoto mwenye umri 0 hadi Miaka 8 anafikia ukuaji timilifu.
Akisoma Hotuba ya Uzinduzi wa programu hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg .Francis Mkuti amesema kuwa Maendeleo katika ukuaji wa mtoto ni matokeo ya afua mbalimbali zinazohusisha wadau wa sekta tofauti .
"Ninyi Washiriki ni wadau muhumu na mkifahamu vizuri hii programu mtawafikishia wazazi na walezi kwenye maeneo yote ya Tandahimba kwa weledi wa hali ya juu," amesema Ndg. Mkuti.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Robert Mwanawima amewasistiza washiriki wa kikao kazi hicho kuzingatia mafunzo hayo kwa umakini ili yalete matokeo yenye tija kwenye jamii.
Kwa upande wa wawezeshaji wameelezea sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto,Umuhimu wa utambuzi wa.mapema.na afua stahiki kwa watoto wenye ulemavu na Muundo wa programJumuishi ua Taifa ya malezi PJT,- MMMAM.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inashughulikia Malezi , Makuzi na Maendeleo ya watoto wadogo kwa kusimamia haki zao zote za msingi ikiwemo afya,ulinzi na usalama wao ambapo kuna jumla ya vituo 26 vya kulea watoto wadogo ambavyo vina watoto 1228,wasichana 697 na wavulana 531
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa