Na Kitengo cha Mawasiliano
Shilingi Milioni Mia tatu thelathini na tatu (333,000,000) zimetumika kutekeleza miradi 177 iliyoibuliwa na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambayo inatekelezwa na walengwa wa TASAF
Fedha hizo zinatekeleza miradi 177 kwa mwaka 2022/2023 kati ya hiyo miradi 117 ya visima vya kuvunia maji ya mvua ambapo kila kisima kina uwezo wa kujaza lita elfu hamsini ( 50,000),miradi 19 ya upandaji wa miti ya matunda na miradi ya barabara ambapo Km 80.197 zimetekelezwa katika vijiji 40
Miradi hiyo hususan ya visima vya kuvunia maji mingi imejengwa katika maeneo ya shule na zahanati ili kuwasaidia katika matumizi mbalimbali ambapo inatekelezwa na walengwa wenyewe wa TASAF wenye umri chini ya miaka 65 ambao wana nguvu ili kuwaongezea kipato
Katika miradi hiyo ipo iliyokamilika na mingine inaendelea ikiwa katika hatua mbalimbali ya utekelezaji
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa