Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepata HATI SAFII katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 baada ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Hii ni mara ya saba mfululizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupata hati safi ya CAG kuanzia mwaka 2015/2016 hadi mwaka wa fedha 2021/2022
Akisoma taarifa Mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mtwara Ndg.Mary Wembe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kupata hati safi (Unqualified Opinion)
Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Maalum la hoja lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri leo Juni 23,2023 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kupata hati safi
Pamoja na pongezi hizo RC amesistiza hoja zilizosalia ziweze kufungwa hasa ambazo majibu yake yapo ndani ya uwezo wa Menejimenti ya Halmashauri na kuzuia hoja mpya
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mariam Mwanzalima katika taarifa yake amesema kuwa hoja zilizobaki Menejimenti inaendelea kufanya jitihada ya kuwasilisha majibu kwa mkaguzi kwa ajili ya uhakiki hatimae ziweze kufungwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa