Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeanza rasmi kutumia mfumo mpya wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ujulikanao kwa jina la Mfumo wa Tausi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma
Akizungumzia mfumo huo Afisa Biashara Ndg.Hamis Natenda amesema kuwa mfumo huu tayari umeanza kufanya kazi ambapo sasa wafanyabiasahara wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wanaweza kupata leseni zao za biasahara popote alipo kwa wakati
“Mfumo huu ni mzuri na hautakuwa na muingiliano wa kifedha kati ya afisa na mfanyabiashara,natoa wito kwa wafanyabiashara kuanza kutumia mfumo huu wa Tausi ambao unarahisisha na kupunguza muda wa kutoka ulipo kufika Halmashauri kulipia leseni na vibali mbalimbali sasa hivi utajisajili mwenyewe kwa kuingia ‘Tausi.tamisemi.go.tz’ na kupata leseni yako huko ulipo,”amesema Ndg Natenda
Naye Mfanyabiashara Salum Mkumba mkazi wa Tandahimba mjini ambaye ametumia mfumo huo kupata leseni yake akiwa nyumbani ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo ambao unawapunguzia wafanyabiashara muda wa kufuata huduma kama vile kulipia leseni na vibali vingine Halmashauri badala yake wanajihudumia wenyewe
Mfumo wa Tausi unaendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ambapo Kabla ya mfumo huu Halmashauri ilikuwa inatumia mfumo wa Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS),i
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa