Na Kitengo cha Mawasiliano
Watumishi na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameshiriki kufanya usafi wa mazingira Katika Hospitali ya Wilaya leo Julai 25,2023 ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa wa Tanzania
Akizungumza mara baada ya kukamilisha shughuli ya Usafi Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndg.Rashid Shaban amewapongeza watumishi na wananchi walioshiriki katika zoezi hilo
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hufanyika kila Mwaka Julai 25 ambapo hutoa fursa ya kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania waliojitolea maisha yao kwa ajili ya kupigania nchi yetu, Maadhimisho hayo Kitaifa mwaka huu yamefanyika Mkoani Dodoma.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa