Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mikorosho 53,360 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imekatwa kuboresha uzalishaji wa zao la korosho ambapo idadi ya miche 33,893 imebebeshwa na miche 30,223 imepandwa ikiwa ni mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Baraza la madiwani wa Halmasahauri ya Tandahimba wakiwa kwenye kikao cha kawaida cha baraza ya robo ya tatu
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji,Afisa Mipango Wilaya Hassan Nzyungu kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika ukumbi wa mikutano ameeleza kuwa ukubwa wa hekta 29.5 imefufuliwa na mashamba yenye ukubwa hekta 655 yameanzishwa
Afisa Mipango Hassan Nzyungu (aliyesimama) akieleza jambo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
Kaimu Afisa Kilimo na Ushirika Haroun Kisimba akijibu swali la Diwani wa Chikongola Yahaya Mussa la kushuka kwa zao la korosho kwa miaka mitatu mfululuzo amesema kuwa sababu mojawapo ni mabadiliko ya tabia ya nchi, mvua kunyesha chini ya milimita 900 imechangia kushuka kwa uzalishaji,mvua za vuli za mwezi wa 9-10 zilisababisha kuangusha maua na korosho changa na uwepo wa mikorosho mizee lakini tayari Halmashauri imechukua hatua kuboresha zao hilo
Wakuu wa Idara na vitengo wakisikiliza kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi wa Halmasahauri
Aidha naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewapongeza madiwani kwa kuendelea kusimamia wananchi katika masuala ya maendeleo na shughuli za kilimo katika kata zao na kusistiza kuwa wataalam wahakikishe pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati
Mkuu wa Wilaya Mhe.Sebastian Waryuba akieleza jambo kwenye baraza la madiwani
Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Tandahimba Baisa Baisa amesistiza ushirikiano uendelee kuimarika kwa Wakuu wa Idara ,madiwani na watumishi ili kuwaletea wananchi wa Tandahimba maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Baisa Baisa akizungumza kwenye baraza hilo
Halmashauri ya Tandahimba kwa upande wa korosho msimu 2018/2019 ilizalishatani 37,650 za korosho ghafi ukilinganisha na tani 37,367 msimu 2019/2020 kwa msimu mwaka 2020/2021 kwa minada 15 ambayo ilifanyika tani 29,433.5 zenye thamani ya Tsh 68,875,132,501.40
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa