Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imevuka lengo la kuchanja Chanjo ya Polio Matone watoto 46137 sawa na asilimia 113.62 wenye umri chini ya miaka mitano katika Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio Awamu ya Tatu ambayo imefanyika kwa siku nne
Akitoa takwimu hizo Sptemba 4,2022 Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dk.Grace Paul amesema kuwa b idadi hiyo imevuka lengo ambalo lilikuwa kuwafikia watoto 40607
“Kampeni imekamilika salama tumevuka lengo la kuchanja watoto zaidi ,lengo lilikuwa kuwafikia watoto 40607 lakini sisi kwa siku nne tumechanja watoto 46137 sawa na asilima 113,”amesema Dk.Paul
Aidha takwimu ya siku ya kwanza walichanja watoto 11090 sawa na asilimia 109.24,Siku ya pili walichanja watoto 12884 sawa na asilimia 126.9,siku ya tatu walichanja watoto 13327 sawa na asilimia 131.27 na siku ya nne ambayo ni mwisho wa Kampeni walichanja watoto 8836 sawa na asilimia 87.03
Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio ya Matone Awamu ya Tatu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) ilianza Septemba 1,2022 na imemalizika Septemba 4,2022
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa