Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetoa Zaidi ya shilingi Milioni 35 motisha kwa walimu ,wanafunzi na shule bora katika maadhimisho ya Juma la Elimu ambalo limeadhimishwa Kiwilaya
Motisha hizo zimetolewa Machi 3,katika maadhimisho ya Juma la Elimu Kiwilaya ambayo yamefanyika katika kiwanja vya shule ya msingi Amani kata ya Tandahimba Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mhe.Kanali Patrick Sawala Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amesema kuwa motisha hizo zimetolewa kwa shule bora,walimu na wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari
Amesema kuwa motisha hizo zimetolewa kwa shule za msingi zilizofaulisha kwa asilimia 100 katika Mtihani wa PSLE mwaka 2022, shule za msingi zenye wanafunzi Zaidi ya 40 zilizopata wastani mzuri wa ufaulu,shule zilizoongeza wastani,shule bora zilizofanya vizuri Kitaluma mwaka 2022,kata bora na wanafunzi waliofanya vizuri sambamba na vyeti vya pongezi
Kwa upande wa Shule za Sekondari wamekabidhi motisha kwa shule bora,walimu, wanafunzi,shule zilizoondoa ziro na shule zilizoongeza ufaulu ambapo wamepata fedha taslimu na vyeti vya pongezi
Akizungumza katika maadhimisho hayo ya Jumala la Elimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa walimu kuendelea kutekeleza mikakati ya Mkoa na Wilaya ili kuongeza ufaulu Zaidi
“Nawapongeza maafisa Elimu wote kuanzia ngazi ya Wilaya hadi kata,walimu na kila mmoja kwa nafasi yake kwa jinsi ambavyo mnafanya kazi kubwa kuhakikisha mikakati tuliyokubaliana inatekelezeka na tunaongeza ufaulu ,”amesema Dc Sawala
Maadhimisho hayo Kimkoa yatafanyika Manispaa ya Mtwara Mikindani Machi 16,2023 ambapo kauli mbiu ya Mkoa “Tuwajibike kwa pamoja,kuleta Maendeleo ya Elimu Mtwara”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa