Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka ametoa msaada wa matibabu kwa kijana Said Abdallah ambaye alipata ajali iliyosababisha kuvunjika kwa miguu miwili na mkono lakini kwa muda wa miezi miwili hakupata huduma stahiki kwa kukosa fedha za matibabu
Akizungumza ofisini kwake Msomoka amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya Mwenyekiti wa Kitongoji chaTandahimba mjini Ashura Madata kutoa taarifa za uwepo wa kijana huyo katika kitongoji chake
Kijana Said Nyecha (29) ambaye aligongwa na gari miezi miwili iliyopita
Amesema kuwa Halmashauri imeamua kumuhudumia kijana huyo ili aweze kupata matibabu stahiki kwakuwa kidonda hicho hakijapata huduma kwa muda hivyo ameamua kuchukua hatua ya kumpeleka Hospitali ya Wilaya kwa hatua za awali na baadaye atampelekwa Hospitali ya Nyangao
“Tumechukua hatua ya kumkatia bima ya ICHF ili aweze kupata huduma nafuu kwakuwa mzazi wakeambaye ni (mama) kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama zake,kwaiyo walipewa matibabu nusu kule Hospitali ya Nyangao sisi tutamalizia fedha yote inayodaiwa hospitali na tutawapa fedha zingine za kuendelea na matibabu sambamba na chakula chake kwa kipindi atakachokuwa hospital,”amesema Msomoka
Naye mama yake Halima Ally amesema kijana wake amegongwa na gari kuanzia mwezi wa pili mwaka huu na gari lilikimbia kwaiyo alipelekwa hospitali kutokana na kukosa fedha hakuweza kupata matibabu mazuri na hivyo kurudi nyumbani
Mratibu wa mfuko wa afya ulioboreshwa (ICHF) Violeth Mahembe akiwakabidhi bima ambayo atapata matibabu bure mgonjwa na mama yake ambayo imelipiwa na Halmashauri
“Naishukuru Halmashauri kwa kumpatia Bima itakayomuwezesha kupata huduma , Mkurugenzi ameridhia kutulipia deni katika Hospitali ya Nyangao ambayo tunadaiwa,kijana wangu amekuwa akiteseka kwa maumivu makali kwakutopata huduma kwa miezi yote miwili,tunaishukuru serikali kwa msaada huu,”amesema Ally.
Hata hivyo mwenyekiti wa kitongoji Ashura Madata ameeleza kuwa hatua hiyo inaonyesha serikali ipo karibu na wananchi wake kwa kuwasaidia pale ambapo wameshindwa kwa kutambua nguvu ya nchi ni vijana
Afisa ustawi wa jamii Gift Limbanga (kushoto)akimkabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi fedha taslimu shilingi laki tano kwa ajili ya kuanzia matibabu (kulia) mwenyekiti wa kitongoji cha Tandahimba Ashura Madata
“Huyu kijana ameteseka,vidonda havikuwa vinasafishwa,mkono umevunjika hajafanyiwa chochote na miguu yote miwili imevunjika kwakuwa uwezo wa mama yake ni mdogo alikuwa anakaa naye nyumbani tu,lakini leo tumepata msaada huu tunaishukuru sana halmashauri yetu kwakuwa Mkurugenzi ametoa gari ili aweze kwenda hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kusafisha na baadaye atapelekwa hospital ya Nyangao,”amesema Madata
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa