Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeshika nafasi ya tatu katika utekelezaji wa afua za lishe kwa mwaka wa fedha 2021l2022 kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Mtwara
Halmashauri imepata ushindi huo baada ya kutekeleza viashiria vya mkataba wa lishe na miongoni mwa viashiria hivyo ni kulipa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano kiasi cha shilingi Elfu moja (1000) ambapo Halmashauri imevuka lengo kwa kulipia kila mtoto shilingi 1528
Fedha hizo hutumika kwa ajili ya matibabu ya watoto wanapogundulika wana utapiamlo lakini pia kwa ajili shughuli za lishe ambazo zinafanyika katika Halmashauri
Mbali na zawadi ya cheti Halmashauri imepokea zawadi nyingine kama vile tape za kupimia watoto na rejesta za kusajiri watoto
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa