Na. Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amekabidhi vitambulisho 2400 kwa Halmashauri ya Tandahimba ili waweze kuvigawa kwa wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ya Wilaya
Akikabidhi vitambulisho hivyo kwa Afisa Biashara Gerald Mmasi,Dc Waryuba amesema kuwa vitambulisho vya mwaka jana vilikuwa na changamoto za hapa na pale lakini kwa mwaka huu vitambulisho hivyo vimerahisishwa kwa kutumia mfumo
Watendaji Kata wakikiliza maelekezo ya ugawaji wa vitambulisho ambavyo kwa sasa vimesajiliwa kwenye mfumo
“Vitambulisho hivi 2400 vikuuzwa kwa wajasiriamali tunataraji tupate shilingi Milioni 48 hivyo jitihada zifanyike ili tumalize vitambulisho hivi ndani ya miezi miwili kwa kuvigawa kwa wajasiriamali wetu wadogo wadogo ili wafanye kazi kwa uhuru,”amesema Waryuba
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machella amesema kuwa pamoja na kupokea vitambulisho hivyo watendaji wa kata (wasajili) wana jukumu la kuhakikisha fedha hizo zinafikishwa kwa wakati
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machella akieleza jambo kwa watendaji kata
“Wasajili mkipokea fedha mzifikishe kwa wakati ili kuepuka vishawishi kwakuwa fedha hizi ni za serikali zinatakiwa zikafanye shughuli mbalimbali za maendeleo ambayo yamekusudiwa,”amesema Machella
Aidha amesema wajasriamali wanatakiwa kuhakikisha wanapata vitambulisho hivyo kwa gharama ya shilingi elfu ishirini ambapo watadumu navyo kwa mwaka mmoja bila kusumbuliwa malipo mengine
Baadhi ya Wakuu wa Idara waliohudhuria makabidhiano hayo ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa