Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 55 kuwalipa fedha ya kujikimu walimu wapya 48 , ununuzi wa magodoro kwa ajili ya walimu hao sambamba na ununuzi wa viti 800 vya walimu wa shule za sekondari na msingi
Viti 800 ambavyo vimenunuliwa kwa ajili ya kukalia walimu wa shule ya msingi na sekondari
Katika Hafla Hiyo Halmashauri imekabidhi vifaa vya kufundishia na kuchezea watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mjimpya Maalum na Mahuta vifaa ambavyo vimetolewa na Ofisi ya Tamisemi pia Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa jiko na bwalo
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akiwa tayari kukabidhi magodoro hayo kwa walimu
Akikabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kuwa anaipongeza Halmashauri kwa jitihhada wanazozifanya kuboresha mazingira kwa Walimu wapya na walimu waliopo
Dc Sebastian Waryuba akimkabidhi mwalimu wa ajira mpya godoro
“Naipongeza Halmashauri kwa hatua hii ya kuwapa motisha walimu wapya magodoro kwa ajili ya kuanza maisha ,hii inawatia moyo wa kufanya kazi lakini hamkuwasahau walimuwaliopo kwakweli tulifanya ziara shule nyingi hawakuwa na viti vya walimu lakini naamini viti hivi vitawasaidia walimu wetu ,”amesema Dc Waryuba
Dc Warryuba (aliyesimama) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji ndugu Said Msomoka
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahaimba ndugu Said Msomoka amesema kuwa fedha hizo zimetoka kwenye mfuko wa Elimu na kila mwalimu amepata godoro moja miongoni mwa 48 ambao 22 ni shule msingi na 26 ni sekondari
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Said Msomoka akiwasistiza waendelee kutekeleza wajibu wao kwa wananfunzi
“Tumefanya haya ili kuwarahisishia walimu hawa wapatae mahali pa kujihifadhi lakini pia viti vitawasaidia walimu katika ofisi zao tulitembelea katika shule mbalimbali tukabaini kuna uhaba wa viti vya walimu kwaiyo tumenunua ili waweze kukaa katika mazingira bora,”amesema Ndg Msomoka
Dc Waryuba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji ndg Msomoka wakimkabidhi kiti mwalimu
Aidha amesema viti 800 vina thamani ya shilingi 27,999,984,magodoro 48 kwa walimu ajira mpya thamani yake shilingi 7,440,000,kiasi cha shilingi 22,892,000 kwa ajili ya posho ya kujikimu kwa walimu wa ajira mpya na kiasi cha shilingi 20,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la wanafunzi wenye mahitaji maalum fedha hizo zimetolewa kwenye mfuko wa elimu
Dc Waryuba akiwakabidhi vifaa vya kufundishia walimu wakuu wa shule ya mahitaji maalum Mjimpya na Mahuta
Hata hivyo walimu wa ajira mpya wameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kuwajali kwa kuwalipa fedha za kujikimu kwa wakati na magodoro hasa katika kipindi ambacho ni wageni katika maeneo ambayo wameripoti
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa