Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amesema kuwa tunatarajia kufungua shule tatu mpya ambazo zinapunguza ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo
Amesema hayo katika ukumbi wa mikuutano wa Halmashauri wakati akizungumza na Wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa
“Kwa mwaka huu tunatarajia kufungua shule tatu mpya ambazo ni Shule ya Sekondari Mndumbwe,Kwanyama na Litehu kwaiyo tutakuiwa na kata tatu ambazo zitakuwa zimepata sekondari ambapo wanafunzi wataanza kusoma Januariu 2023,”amesema Mkurugenzi
Aidha amesema katika kata 32 zitabaki kata mbili ambazo hazitakuwa na sekondari ambazo ni Kata ya Mahuta na Mkwedu ambapo amebainisha kuwa kata ya Mahuta tayari ipo katika mpango wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kwaiyo itabaki kata moja ya Mkwedu kati ya kata 32
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa