Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri 184 za Tanzania bara zitanufaika na mradi wa BOOST katika kuboresha Elimu ya Awali na Msingi kwa kujenga miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo ambapo mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano
Akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uelewa wa kusimamia miradi hiyo ya BOOST Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Mwl. Kiduma Mageni amesema mafunzo hayo ni muhimu ili kutekeleza miradi hiyo katika viwango vya ubora na muda unaotakiwa
Mafunzo hayo yamefanyika Disemba 22- 23,2022 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ualimu Kawaida Manispaa ya Mtwara Mikindani na kujumuisha Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi na Mtwara
Aidha Mwl Mageni ameeleza kuwa BOOST ni mpango wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu Msingi hivyo washiriki ni muhimu kusimamia miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa Halmashauri husika
Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu TAMISEMI Ndg.Vicent Kayombo amewapongeza washiriki kwa kupata mafunzo hayo na kuwasistiza kuendelea kuhamasisha wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wote wenye sifa ya kuanza Elimu ya Awali na Msingi
Mradi wa Boost ni sehemu ya mpango wa Lipa kutokana na matokeo katika Elimu EP4R II ambao umelenga kutekeleza afua nane muhimu kwa muda wa miaka mitano ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.15 zitatumika katika utekelezaji wa mradi wa BOOST kwa kujenga vyumba vya madarasa Elfu kumi na mbili (12000) na matundu ya vyoo katika shule elfu kumi na saba mia moja themanini na mbili (17182) katika Halmashauri zote 184
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa